1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Wapalestina wapata serikali mpya

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHv

Serikali mpya ya Palestina imeapishwa na rais Mahmoud Abbas baada ya bunge la wapalestina kuidhinisha serikali hiyo ya mseto ya vyama vya Hamas na Fatah.

Hapo awali waziri mkuu mteule bwana Ismail Haniya aliliambia bunge kuwa serikali yake itaendelea kutekeleza hatua ya kusimamisha mapambano na Israel. Lakini bwana Haniya amesema , harakati za kupinga kukaliwa maeneo ya wapalestina ni jambo halali.

Na rais Mahmoud Abbas wa mamlaka ya Palestina amesema kuwa anapinga aina zote za matumizi ya nguvu lakini ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa juu ya kuanza tena kuisadia Palestina kwa fedha.

Marekani imeitikia habari juu ya kuapishwa serikali hiyo kwa upoovu na kusema kuwa hotuba ya waziri mkuu Ismail Haniya inavunja moyo na kwamba msimamo wake juu ya kusisitiza haki ya wapalestina ya kupinga kukaliwa maeneo yao ni jambo la usumbufu.

Na Israel imeikataa kabisa serikali hiyo ya mseto iliyoundwa kutokana na vyama vya Hamas na Fatah.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umeikaribsha serikali hiyo mpya ya wapalestina lakini umesema kuwa hatua ya kuanza tena kuwasaidia wapalestina kwa fedha itategemea na matendo ya serikali hiyo.

Na Norway imesema kuwa itaanzisha tena uhusiano wa kisiasa na kiuchumi na serikali mpya ya Palestina. Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo ameeleza kuwa serikali ya mseto ya vyama vya Hamas na Fatah inachukua hatua zenye lengo la kutekeleza matashi ya jumuiya ya kimataifa.