1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini-Obama na Georgia:

27 Agosti 2008

Kampeni ya uchaguzi wa rais ya marekani na hatima ya Obama pamoja na mzozo wa Georgia ndio mada kuu:

https://p.dw.com/p/F5jp

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani umeegemea zaidi hii leo mada 2: mvutano kati ya Georgia na washirika wake wa magharibi na Russia iliozitambua jana rasmi kama nchi huru -maeneo ya Georgia ya Abchazia na kusini mwa Ossetia.

Mada nyengine ni kutawazwa kwa Barack Obama kama mtetezi rasmi wa wadhifa wa urais wa Marekani .

Gazeti la Volksstimme kutoka Magdeburg juu ya uchaguzi wa rais wa Marekani:

►◄"1984 mtetezi wa haki za kiraia Jesse Jackson,alizusha msdisimko alipogombea kiti cha urais na akatokea watatu katika watetezi wa chama cha Democratic party.Robo karne baadae, Barack Obama ,mweusi mwengine ndipo ameibuka mtetezi rasmi wa chama kugombea urais wa Marekani.

Biramu lake la "mabadiliko" bila shaka limewagusa sana wamarekani.Kwani, bila kujali rangi yake ,baada ya miaka 8 ya george Bush katika ikulu,yadhihirika wakati umewadia wa kuleta mabadiliko.

Lakini,kila tarehe ya uchaguzi ikikaribia,Obama anazidi kuishiwa na pumzi.Miongoni mwa m abwnyenye wa kizungu wanajiuliza kwa wasi wasi,Obama anakusudia mageuzi gani ?

Ndio wanakubaliana na kumteketeza Bush na sera zake.Lakini wapi seneta wa Illinois anakotaka kuongoza Marekani ? Je, muamerika-mweusi aweza kutuhakikishia maisha yetu bora ?

Jibu lake litaonekana siku ya kupiga kura kujua iwapo wakati kweli umewadia wa mageuzi ya kweli nchini Marekani-kumtawaza sasa kitini rais-mweusi."

Likiendeleza mada hii,gazeti la BRAUNSCHWEIGER ZEITUNG laandika kwamba, hata kivuli hurudi tena:

Kwa jinsi inavyoonekana ni kana kwamba ni marudio ya historia kuwa muda mfupi kabla Edward Kennedy kuhutubia,watu kadhaa walitiwa nguvuni kwa kutiliwa shaka ya kutaka kumuua.hata katika mkutano huu wa sasa wa chama uvumi umeenea kuwa barack Obama -anaeonekana kuwa alama ya matumaini na ya kuachana na siasa za kizamani alizoitosa George Bush Marekani,atolewe mhanga. Barack atafaulu iwapo atavuka salama changamoto hii.

Likitugeuzia mada,gazeti la Badische Zeitung kutoka Freiburg linauchambua msimamo wa Russia juu ya mzozo wa Georgia:Laandika:

"Kwa kujitenga kwa majimbo 2 ya georgia,Russia inapiga mfano wa kufuatwa ambao Russia binafsi ilivinjari kwa miaka kadhaa usifuatwe katika jimbo la Chechnia. Rais Medwedew wa Russia, yamkini akaja kutia goli katika lango lake mwenyewe.Kwa upande mwengine,kuna wakaazi wachache wa jamii za kirusi katika nchi zanachama wa umoja wa Ulaya ulaya ya mashariki na hata Ukraine ambao wanabidi kulindwa.Hapa tunakumbushwa usemi wa wahenga kuwa dola kuu haziporomoki kwa amani-ukweli ambao waweza ukadhihirika.

Gazeti la Schwąbische Zeitung laona kwamba Russia hivi sasa inataka kuuchafua kabisa uhusianmo wake na kambi ya magharibi.Laandika:

"Abchasia na kusini mwa Ossetia zifuate mfano wa Kosovo na mara hii goli limetiwa katika lango la kambi ya magharibi.

Vigogo vya Moscow vinatoa changamoto jinsi vinavyoweza kuichokoza Marekani na Umoja wa Ulaya.Hii pia ni kuwatia kitunga cha macho wananchi wa urusi kuamini dola lao kuu la Urusi lililozama sasa limeibuka tena.

Kwamba katika ulimwengu huu wa biashara ya utandawazi,watakuja kujuta majuto mjukuu,hakuna anaewaza hayo huko Kremlin.