1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GERONA: Nchi za Ulaya ziongoze juhudi za amani

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrz

Hispania,Ufaransa na Italia zimezindua mradi unaohusika na juhudi za kutafuta amani katika Mashariki ya Kati.Nchi hizo zimesema,Ulaya lazima iongoze juhudi za kukomesha machafuko,hasa kati ya Wapalestina na Waisraeli.Waziri mkuu wa Hispania Jose Luis Rodriguez Zapateri,akiwa mwenyeji wa mkutano huo mjini Gerona,amesema ni matumaini yake kuwa Ujerumani na Uingereza pia zitashiriki katika mradi huo unaotoa mwito wa kuwa na tume ya kuchunguza hali ilivyo.Baadae kufanywe mkutano wa amani utakaoingiza pande zote za mgogoro na vile vile kuchukuliwe hatua ya kubadilishana wafungwa.Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi,akizungumza kutoka Rome amesema, mradi huo ni muhimu katika juhudi ya kukomesha mateso yasiovumilika.