1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHAZNI:Juhudi zakutafuta sehemu ya kufanyika mazungumzo zaendelea

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcA

Serikali ya Afghanistan na wateka nyara wa kundi la Taleba hii leo wanajadiliana mahali pa kufanyika mazungumzo ya ana kwa ana juu ya kuachiwa kwa mateka 21 wa Korea Kusini wanaoshikiliwa zaidi ya wiki mbili sasa na kundi hilo la Taleban.

Ujumbe wa Serikali ya Korea Kusini umekwenda katika jimbo la Ghazni kusini magharibi mwa Kabul wanakoshikiliwa mateka hao, kujaribu kutafuta uwezekeno wa kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana.

Kundi hilo la Taleba linataka mazungumzo hayo yafanyike kwenye eneo lililochini ya himaya yao na wamehakikisha usalama kwa ujumbe wa Serikali ya Korea Kusini.

Vinginevyo msemaji wa kundi hilo amesema kuwa, vikosi vya usalama vya umoja wa mataifa vilinde usalama katika eneo lingine litakalopendekezwa.

Kwa upande wake Rais Hamid Karzai wa Afghanistan alielezea nia ya serikali yake katika mzozo huo.

OTON:KARZAI

Karzai anasema kuwa serikali yake inataka wakoreahao waachiwe kwa usalama na analaumu kuwa watekaji nyara hao ambao anasema wengi wao ni raia wa nje ya afghanistan wanaipa jina baya nchi hiyo kwa kitendo hicho.

Wakati huo huo msemaji wa Polisi katika jimbo hilo amesema kuwa wamefanikiwa kupeleka madawa kwa ajili ya mateka wanawake 18 na wanaume wawili, lakini watekaji hao wamekataa ombi la serikali ya Afghanistan kupeleka madaktari kuwatibu mateka.

Tayari watekaji hao wamekwishawaua mateka wawili kati ya 23 iliyowateka.

Katika hatua nyingine Serikali ya Afghanistan imesema kuwa zaidi ya wanamgambo 100 wa kitaleban wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na majeshi ya Marekani huko katika jimbo la kusini la Helmand.