1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Goma, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Makubaliano ya kusitisha mapigano bado yanafanyakazi.

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTc

Makubaliano tete ya kusitisha mapigano yanaendelea kufanyakazi mashariki mwa DRC hadi jana Jumamosi wakati wawakilishi wa umoja wa Ulaya wamehimiza ushirikiano zaidi baina ya nchi hizo jirani za Rwanda na Kongo.

Mwakilishi maalum wa umoja wa Ulaya katika eneo la maziwa makuu, Roeland van de Geer, ameliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano kuwa wanawasiwasi na hali katika eneo la mashariki ya DRC. Ameongeza kuwa wana matumaini kuona uwajibikaji kutoka mataifa ya eneo hilo na utekelezaji.

Wito huo unafuatia wimbi la mapigano ya hivi karibuni mashariki ya DRC katika jimbo lenye machafuko la Kivu kaskazini kati ya majeshi yanayomuunga mkono jenerali muasi Laurent Nkunda na majeshi ya serikali pamoja na wapiganaji kutoka Rwanda.

Wanajeshi kadha wa DRC wameuwawa katika mapigano hayo, yaliyoelezwa kuwa ni makubwa sana , siku ya Ijumaa na ujumbe wa umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini DRC , unaojulikana kama MONUC.