1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guardiola ashangazwa na timu yake

Sekione Kitojo
5 Machi 2018

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hajawahi kufikiria timu yake itakuwa mbele katika pointi ikifukuzia ubingwa katika Premier League kama inavyofanya mwaka huu.

https://p.dw.com/p/2tjVe
FC Basel gegen Manchester City - UEFA Champions League
Picha: Getty Images/S.Bozon

Sasa inahitaji  ushindi  mara nne  tu  katika  michezo  9  ya  mwisho  kujihakikishia  ubingwa. Kuweka  umbali  wa  pointi 25 dhidi  ya  Chelsea, 33  dhidi  ya Arsenal. Tottenham, Liverpool  na  Manchester United , zilipata matokeo  mazuri na  kuweka  kasi  nzuri. Hadi  sasa  tuko  vizuri, nafikiri  ni  kutokana  na  vile  tunavyocheza. Vile  tunavyocheza  hivi sasa  kidogo  ni  sawa na  kile  tulichofanya msimu  huu,"  alisema Pep Guardiola.

Ikiwa imebakia  michezo 9 kumaliza msimu , City ambayo  ina  pointi 78 , ina  nafasi ya  kuwa  timu  ya  kwanza  kufikisha  pointi 100 katika  historia  ya  ligi  ya  England.

Premier League, Josep Guardiola, Trainer Manchester City
Guardiola amejenga kikosi imara uwanjani EtihadPicha: picture-alliance/AP Photo/E. Lukatsky

Nae  kocha  wa  Manchester United Jose Mourinho amesema Marcus Rashford anapata  uzoefu  anaohitaji  kusonga  mbele  na ukweli kwamba  hajaanza  mchezo  katika  kikosi  cha  kwanza  tangu Desemba  haitaathiri  nafasi  yake kuteuliwa  katika  kikosi  cha  taifa katika  kombe  la  dunia.  Vyombo  vya  habari  vya  Uingereza vimeripoti  kwamba  hali  hiyo  inasababisha  kocha  Southgate kupata  wasi  wasi  wakati  akijitayarisha  kutaja  kikosi  chake kwa ajili  ya  michezo  ya  kirafiki dhidi  ya  Uholanzi na Italia.

Mchezaji  wa  zamani  wa  Arsenal  Thiery Henry  amesema  hata kataa changamoto, iwapo  nafasi  itajitokeza  kumrithi Arsene Wenger  kuwa  kocha  wa  washika  bunduki  Arsenal.

Hata  hivyo , Henry ana  shauku  kwa  raia  mwenzake  wa  Ufaransa ambaye  yuko  katika  kikaango , kuwa na  "usemi  wa  mwisho" kuhusu kazi  hiyo  katika  Arsenal  ambayo  ilianza wakati  Wenger alipoanza  kazi  ya  kuifunza  klabu  hiyo  ya  magharibi  mwa  London mwaka  1996.

Minong'ono  ya  muda  mrefu  kuhusu  nafasi  ya  Wenger  katika Arsenal  iliongezeka  baada  ya  kipigo  cha  nne  mfululizo  katika michezo  yote  na  kipigo  cha  mabao 2-1  ugenini  dhidi  ya Brighton jana  imezidi  kusogeza  karibu  majaali  yake  ya  kuondoka katika  klabu  hiyo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo /  dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf , Saumu