1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za binadamu China.

Abdu Said Mtullya26 Februari 2009

China yapinga ripoti ya Marekani inayoilaumu vikali nchi hiyo kwa kukiuka haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/H1OM
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton akisalimiana na rais Hu Jintao wa China. Wizara yake imeilaumu China kwa kukiuka haki za binadamu.Picha: AP

WASHINGTON.

Marekani imeilaumu China, vikali kwa kukiuka haki za binadamu , wiki moja baada ya waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton kufanya ziara nchini China ambapo hakusema kitu juu ya suala hilo

Katika ripoti yake ya kila mwaka juu ya haki za binadamu duniani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imeilaumu Urusi ambako imesema haki za raia zinabanwa.

Lakini China imesema kuwa ripoti hiyo haina msingi.

Ripoti hiyo pia inatilia maanani mfumuko wa sheria zinazoyabana makundi yasiyo ya kiserikali katika sehemu mbalimbali za dunia.