1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za Wasichana

13 Machi 2014

Wanawake barani Afrika wamekuwa na nguvu nyingi katika miaka iliyopita na hata kushika nafasi za uongozi. Licha ya hilo, wasichana wengi bado wanapambana na ubaguzi. Safari ya kufikia usawa wa kijinsia bado ni ndefu.

https://p.dw.com/p/19O9a
Wasichana darasani (Picha: picture alliance/ausloeser-photographie).
Picha: picture alliance/ausloeser-photographie

Baada ya kupokea barua nyingi za kusifu kipindi cha kwanza cha Noa Bongo Jenga Maisha Yako kilichohusu wanawake na wasichana na ambacho shujaa wake Bibiye alizungumza wazi kuhusu ubaguzi wa wanawake katika maisha ya kila siku na kuwahamasisha rafiki zake wapinge jambo hilo, Deutsche Welle imeamua kutayarisha mfululizo mpya wa vipindi kuhusu haki za wasichana.

Wakati huu tutafuatana na marafiki watatu - Ciro, Fatuma na Cheptoo - wanapokabiliana na changamoto za usichana. Katika kupitia visa mbali mbali, marafiki hao watafahamu zaidi kuhusu haki zao na jinsi ya kupambana na hali ngumu. Sikiliza ufahamu zaidi kuhusu haki za msichana na kupata umakini kuhusu jambo hilo.

Vipindi vya Deutsche Welle vya Noa Bongo! Jenga Maisha Yako vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamhara.