1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za wenyeji asilia Australia

Abdu Mtulya13 Februari 2008

Waziri Mkuu wa Australia Kevin Rudd amewaomba radhi wenyeji wa Australia-Aborigines kwa maonevu yaliyowafika watu hao kwa muda wa miaka mingi

https://p.dw.com/p/D75t
Waaborigines wakisheherekea nje ya bunge baada ya waziri mkuu kuomba radhi.Picha: AP

Hatua ya waziri mkuu huyo imefungua ukurasa mpya katika uhusiano baina ya wanyeji hao na serikali ya Australia.


Akizungumza bungeni,kuwaomba radhi rasmi wenyeji asilia wa Australia, waziri Mkuu Rudd amesema mjini Canberra kuwa sheria na sera za nchi zilisababisha, uchungu na maonevu kwa watu hao ,kwa muda wa miaka mingi.

Amesema samahani kwa watu hao ,kwa mateso na dhulma iliyowafika.

Waziri Mkuu Rudd amesema wakati sasa umefika wa kufungua ukarasa mpya katika historia ya Australia kwa kusahihisa makosa waliyofanyiwa wenyyeji wa nchi hiyo, ili kuweza kusonga mbele kwa nia safi.

Katika hotuba yake waziri mkuu huyo pia aliomba samahani kwa niaba ya mabunge na serikali zilizopita nchini Australia kwa kutekeleza sera zilizosababisha maonevu makubwa kwa wakazi asilia wa nchi hiyo.