1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna maafikiano kuhusu mustakabali wa Kosovo

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZ1O

Wapatanishi wa kimataifa wameshindwa kuafikiana juu ya mustakabali wa jimbo la Serbia la Kosovo.Ripoti iliyotayarishwa na wanadiplomasia wa kundi la pande tatu la Umoja wa Ulaya,Marekani na Urusi na kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon imesema,majadiliano ya miezi minne hayakufanikiwa kupata makubaliano. Kwa upande mwingine,Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa,Vitaly Churkin ametoa wito wa kuendelea na majadiliano ya kundi hilo.

Wakosovo wenye asili ya Kialbania ambao ni wengi katika jimbo hilo la Serbia wanataka uhuru na huenda hata wakajitangazia uhuru wao,hatua inayopingwa na Belgrade.Kwa upande mwingine, Shirika la Kujihami la Mataifa ya Magharibi NATO,limeahidi kubakisha kikosi chake cha amani cha wanajeshi 16,000 katika jimbo hilo la Serbia,Kosovo.