1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna uwajibikaji wa watuhumiwa wa ubakaji wa UN - Ripoti

Grace Kabogo
15 Septemba 2017

Nyaraka za uchunguzi zinaonesha kuna hali ya kutowajibika panapohusika na madai ya visa vya ngono vilivyofanywa na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika Kati.

https://p.dw.com/p/2k2qj
Zentralafrikanische Republik Bangui MINUSCA UN Truppen
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Ripoti hiyo ni ukosoaji wa hivi karibuni kabisa kuhusu jinsi visa vya ngono vilivyochunguzwa katika nchi hiyo mwaka jana, ambako Umoja wa Mataifa ulikuwa na ujumbe mkubwa kabisa wa kusimamia amani duniani.

Visa 14 vilichunguzwa katika kampeni ya Umoja wa Mataifa, lakini kikundi hicho cha uchunguzi kinasema katika visa vinane kwenye orodha hiyo, wahanga hawakuhojiwa.

Pindi madai hayo yatakapothibitika kuwa na ukweli, nchi wanakotoka wahusika zitakuwa na wajibu wa kuwafungulia mashtaka.