1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali imeendelea kuwa tete nchini Syria

1 Agosti 2011

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza mbinyo zaidi dhidi ya Syria kufutia matukio ya ukandamizaji dhidi ya waandamanji nchini humo ambapo watu 140 wameuwa.

https://p.dw.com/p/127Kt
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William HaguePicha: AP

Akizungumza na Shirika la Habari la Uingereza BBC, Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema kunahijitika shinikizo zaidi kutoka nchi nyingine na wala si za magharibi tu pekee.

Pamoja na kusema kusiwepo hatua za kuingilia kijeshi, William Hague, ameyataja mataifa ya Kiarabu ikiwemo Uturuki kufanya jitihada zaidi katika kufanikisha jambo hilo.

Uingereza sambamba na Ufaransa, Ujerumani, Ureno na Marekani kwa namna fulani zimekuwa wakishinikliza umoja wa mataifa ulaani machafuko yanayoendelea nchini Syria.

Lakini Urusi, China, Afrika Kusini, India na Brazil ambazo zimegadhabishwa na kampeni ya NATO nchini Libya, zimekaidi kuunga mkono hatua hiyo. China na Urusi zimetishia kutopiga kura azimio lolote dhidi ya Assad.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema wanataka kuona vikwazo zaidi na kwamba wamekubaliana vikwazo vingine kwa upande wa Umoja wa Ulaya, ambavyo kwa ufafanuzi zaidi vitatangazwa wiki hii.

Aliongeza kwa kusema angalipenda kuona Umoja wa Mataifa unalaani ukandamizaji huo, kutoa wito wa kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa na kutoa wito wa haki ya kusikilizwa kwa malalamiko.

Hata hivyo Waziri Hague alikiri kuwepo kwa mgawanyiko katika baraza la usalama na kusema hali hiyo inachanganya sana na kusababisha ugumu katika kufikia maamuzi.

Syrien eingestellt 01.08.2011
Vurugu nchini SyriaPicha: picture-alliance/abaca

Katika hatua nyingine, kumetolewa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya watu karibu 140 kuuwawa ikiwa ni tukio kubwa zaidi kutokea tangu kuanza kwa maandamano ya kuupinga utawala wa nchi hiyo miezi minne iliyopita.

Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema vifo hivyo vinajumisha vile vya watu karibu 100 waliowawa na vikosi vya usalama katika kitovu cha maandamano hayo huko katika mji wa Hama.

Mji huo pia uliwahi kutokea vurugu nyingine 1982, zilizohusisha vikundi vya kiislamu, ambapo inakasiwa karibu watu 20.000 waliuwawa.

Wanaharakati wanasema idadi ya watu waliouwawa inaweza kuongezeka kutokana uwepo wa watu wengi zaidi waliojeruhiwa.

Rais Barack Obama wa Marekani na viongozi wa Umoja wa Ulaya wamelaani mauwaji hayo wakati Ujerumani na Italia zimetoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mkutano huo unaweza kufanyika baadae leo ingawa inahisiwa kunaweza kutokea mgawanyiko mkali miongoni mwa nchi wanachama ambazo hazijakubaliana hata kuhusu kutoa kauli juu ya ukandamizaji wa Rais Bashar al-Assad dhidi ya upinzani.

Mwandishi: Sudi Mnette/ AFP
Mhariri: Abdul-Rahman