1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali katika Kosovo

Oumilkher Hamidou4 Januari 2009

Nato na Umoja wa Ulaya wapania kuzuwia fujo Kosovo

https://p.dw.com/p/GRix


Jumuia ya kujihami ya NATO na Umoja wa Ulaya zimezidisha idadi ya vikosi vyao vya usalama ili kukabiliana na machafuko yaliyoripuka katika eneo la kaskazini la Kosovo.Wazima moto wasiopungua sita wamejeruhiwa katika shambulio la bomu,walipokua wakijaribu kuzima moto katika maduka mawili ya waalbania, yaliyoripuliwa na waserbia katika  mji wa Mitrovica.Vikosi ziada vya kulinda amani vya KFOR na maafisa wa polisi wa kikosi cha EULEX wamewekwa mjini humo.Mashambulio hayo yamepamba moto baada ya kuuliwa kiijana wa kiserbia jumanne iliyopita.