1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ngumu ya kusubiri kwa Merkel katika uchaguzi wa Hesse

Sekione Kitojo
28 Oktoba 2018

Mabadiliko ya ngome za kisiasa Ujurumani yanatarajiwa kulikumba jimbo la pili katika uchaguzi wa majimbo leo Jumapili(28.10.2018), na  kutishia mtikisiko mpya kwa serikali kuu ya mjini  Berlin,inayoongozwa na Merkel.

https://p.dw.com/p/37HGa
Hessen Lich, Landtagswahl
Picha: Getty Images/M. Gottschalk

Serikali  kuu  iliyoko  katika  mji  mkuu  Berlin imeshusha  pumzi tangu  pale  wakaazi  wa  jimbo  la  Bavaria  walipouwaadhibu washirika  wa  Merkel , chama  cha  kihafidhina  cha  Christian Social Union CSU  na  kile  cha  siasa za  wastani  za  mrengo  wa kushoto  cha  Social Democratic  SDP, katika  uchaguzi  wa  jimbo mapema  mwezi  huu.

Landtagswahl in Hessen Ginsheim-Gustavsburg
Wapiga kura wanaendelea kupiga kura katika uchaguzi wa jimbo muhimu la Hesse(28.10.2018)Picha: Getty Images/AFP/T. Silz

Kikilenga  kupuuzia  vita  vya  ndani  ambavyo  vimesababisha kuwakimbiza  wapiga  kura  kutoka  vyama  vikuu   vitatu  vya  asili, viongozi wametoa  wito  wa  kuwa  na  nidhamu  na  bila  kufukuzana kabla  ya  uchaguzi kuanza  mapema  leo, ambapo  watu  milioni  4.4 wana  haki  ya  kupiga  kura  katika  jimbo  la  Hesse, ikiwa  ni asilimia  saba  tu  ya  wapiga  kura  nchi  nzima.

"Je Hesse  itaripua serikali  ya  inayojulikana  kama  "ushirika mkuu"?  mjini  Berlin  kati  ya  chama  cha  kansela  Merkel  cha Christian Democratic Union CDU  na  kile  cha  SPD , gazeti linalouzwa  zaidi  nchini  Ujerumani  la  Bild  limeuliza.

"Hesse  yapiga  kura , Berlin yatetemeka," limeandika  gazeti  la Sueddeutsche Zeitung.

"Kansela  hajawahi  kuwa  katika  mbinyo  mkubwa  kama  huu."

Hessiche Ministerpräsident Volker Bouffier und seine Frau Ursula
Waziri mkuu wa jimbo la Hesse Volker Bouffier na mkewe UrsulaPicha: DW/K. Brady

Matokeo  mabaya

Matokeo  mabaya  kwa  ama  CDU ama  SPD yatafungua  duru mpya  ya  kuelekezana  vidole na  miito  ya  kuachana  na  "ushirika mkuu"  wa  tatu  wa kansela  huyo  wa  muda  mrefu  usio  na mapenzi  ya  kweli."

Wengi  katika  jimbo  la  Hesse kwa  kiasi  kikubwa  wanaridhika  na serikali  yao  ya  jimbo, ikiwa  na  maana  "hakutakuwa  na  hali inayoelekeza  mabadiliko  miongoni  mwa  wapiga kura  wa  Hesse bila  nia  ya  kutuma  ujumbe  mjini  Berlin," gazeti  la  kila  wiki  la Die  Welt am Sonntag  limeeleza  katika  maoni  yake.

Ishara  ya  kwanza  ya  kuporomoka  kwa  Merkel  itakuja  saa  12 jioni  saa  za  Ulaya  ya  kati  wakati  vituo  vya  kupigia  kura vitakapofungwa  na  matokeo  ya  kwanza  kuonekana.

Deutschland, Fulda: Der hessische Ministerpräsident Volker Bouffier Bundeskanzlerin Angela Merkel nehmen an der letzten Wahlkampagne vor den bevorstehenden Landtagswahlen teil
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) na waziri mkuu wa jimbo la Hesse Volker Bouffier (kulia)Picha: REUTERS

Uchunguzi  unaelekeza  kwa  waziri  mkuu  wa  jimbo  hilo  kutoka CDU  na  mfuasi  mtiifu  wa  Merkel  Volker Bouffier  na  mpinzani wake  kutoka  chama  cha  SPD Thorsten Schaefer-Guembel wakipata  vipigo  vikubwa  ikilinganishwa  na  mwaka  2013.

Vyama  vyote  viwili  vinatarajiwa  kupoteza  kiasi  ya  alama  10, katika  matokeo  ambayo CDU inaweza  kupata  juu  ya  20   na karibu  na  20 asilimia  kwa  SPD.

Kutegemea  vipi  vyama  hivyo  vitaweza  kufanya  katika  uchaguzi huo, hesabu  za  vyama  hivyo shirika katika  serikali  kuu  zinaweza kuruhusu  ama  kuongoza serikali  mpya  ya  jimbo, na  kuwapa Merkel  ama  kiongozi  wa  SPD Andrea  Nahles  ushindi  wa kiishara.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

mhariri: Grace Patricia Kabogo