1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Mashariki ya kati.

Mutasa24 Mei 2007

Serekali ya Israel imewakamata zaidi ya watu 30, viongozi wa kundi la Hamas mkiwemo pia waziri moja

https://p.dw.com/p/CB3z
Makombora kutoka eneo la Gaza yakilenga Israel
Makombora kutoka eneo la Gaza yakilenga IsraelPicha: AP

Israel inasema imechukua hatua hii ili ujumbe uyafikie makundi ya kigaidi ya wapalastina yanayo endelea kuvurumisha maroketi ndani ya Israel, yakomeshe hujuma zake.

Oparesheni ya kamata kamata viongozi wa Hamas, ilifanyika jana usiku katika mji wa Nablus , ukingo wa magharibi, ambapo Miongoni mwa watu 33 wafasi wa Hamas waliokamatwa, alikuemo waziri wa Elimu wa

Palastiana Nasseredin Al-Shaer, wabunge wa tatu wa Bunge la Palastina, pamoja na Ma Meyor saba wa miji ilioko kwenye ukingo wa Magharibi.

Waziri wa ulinzi wa Isarel, Amir Peretz amekiambia kituo cha redio ya jeshi la Israel, hatua waliochukua kuwakamata wafasi hao wa Hamas, ambao wanaunda Serekali ya umoja wa Taifa la Palastina, ni kuufikisha ujumbe kwa makundi ya wapiganaji wa kipalastina yanayo endelea kurusha makombora ndani ya Israel, yasitishe hujuma zake.

Serekali ya Palastina imekilaumu kitendo hicho cha kuwakamata viongozi hao wa Hamas ambapo waziri wa Habari wa Palastina Mustafa Barghouti amesema huo ni Utekajinyara, kuuwa Demokrasia ya wapalastina na hujuma dhidi ya taasisi za Mamlaka ya wapalastina.Waziri Barghouti ameitaka jumuia ya kimataifa iingilie kati mzozo huu.

Kukamatwa kwa viongozi wa Hamas kunafanyika wakati mashambulizi ya ndege za kivita za Israel yakiendelea ndani ya Palastina kwa wiki moja unusu sasa, wapiganaji wa Hamas 25 kuwawa, wakiwemo pia raia 12 wa palastina

Hata hivo wapiganaji wa Hamas nao wameapa kuendelea na mashambulizi yao ya makombora dhidi ya Israel.

Zaidi ya makombora 130 yamevurumishwa na kundi la Hamas dhidi ya Israel , Misrael moja kufariki, na 16 kujeruhiwa, huku Mamia ya wa Israel wakiukimbia mji wa Sderot.

Katika mashambulizi ya jana usiku wapalastina 7 walijeruhiwa vibaya, tukio ambalo Israel ilisema walilenga vituo viwili vya kubadilishia fedha abavyo vimekua vikitumiwa na wapiganaji wa Hamas kupokea pesa wanazotumiwa kutoka njee.

Kwa vyovyote vile huu ndio mwanzo wa Viongozi wa Isarel kuwakamata na kuwahujumu viongozi wa Hamas kama

walivo sema mapema wiki hii.

Tayari kuna viongozi wa Hamas 39 waliokamatwa mwaka jana, ambao bado wamo katika magereza ya Israel.