1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg , Ujerumani. Wapinzani wa Utandawazi wafanya ghasia.

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx5

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga utandawazi wamefanya maandamano katikati ya mji wa kaskazini ya Ujerumani wa Hamburg wakipinga mkutano wa mawaziri wa umoja wa Ulaya na wa mataifa ya bara la Asia.

Waandamanaji hao waliweka vizuwizi barabarani na polisi walijibu kwa kuwashambulia kwa mabomba ya maji na virungu baada ya kurushiwa chupa na mawe.

Polisi wamesema kuwa watu 24 wamekamatwa.

Maandamano hayo yamefanyika katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku mbili kati ya mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya na mataifa ya Asia. Mada ambazo zilipangwa kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na mzozo wa Iraq, Afghanistan na mashariki ya kati pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.