1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamilton ashinda Canadian Grand Prix

8 Juni 2015

Dereva Lewis Hamilton aliibuka kidedea katika mashindano ya Canadian Grand Prix na kisha akakiri kuwa alihihitaji ushindi huo. Huo ulikuwa ni ushindi wake wa nne katika mashindano saba ya msimu huu.

https://p.dw.com/p/1Fdg6
Kanada Montreal Formel 1 Lewis Hamilton
Picha: Getty Images/AFP/J. Samad

Hamilton alifadhaishwa na matukio ya mashindnao yaliyopita ya Monaco baada ya kutofanikiwa kushinda kufutia makosa yaliyosababishwa na kikosi chake cha Mercedes.

Mwenzake Nico Rosberg ambaye alipta ushindi wa Monaco, almaliza katika nafasi ya pili hapo jana wakati Valtteri Bottas akimaliza katika nafasi ya tatu, na hivyo kuipa timu ya Williams fursa ya kupanda jukwaani kwa mara ya kwanza msimu huu.

Mkuu wa timu ya Mercedes Toto Wolff, amesema wamekuwa na wiki mbili ngumu kutokana na ukosoaji mkubwa walioupata kutokana na makosa ya Monaco ambayo yamepelekea kufanya tathmini kuhusiana na maamuzi ya kiufundi ya mbio.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu