1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamilton na Rosberg kuwania ubingwa wa ulimwengu

Admin.WagnerD21 Novemba 2014

Baada ya mapambano 18 ya mwanzo msimu huu, pambano la kuwania ubingwa wa mashindano hayo litaamuliwa Jumapili Abu Dhabi kati ya Lewis Hamilton na Nico Rosberg madereva wa magari ya Mercedes.

https://p.dw.com/p/1DrKQ
Nico Rosberg und Lewis Hamilton
Picha: picture-alliance/dpa/Daniel Dal Zennaro

Dereva huyo Nico Rosberg akishinda atakuwa dereva wa tatu wa Ujerumani kutwaa taji hilo baada ya Michael Schumacher na Sebastian Vettel.

Hamilton yuko mbele ya Rosberg kwa pointi 17 na iwapo atashika nafasi hata ya pili tu basi atatawazwa kuwa bingwa msimu huu. hamilton amesema kuwa hataruhusu kufanya kitu chochote cha kijinga katika kinyang'anyiro hicho muhimu mjini Abu Dhabi siku ya Jumapili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Khelef