1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Amri ya kutopandisha bei za bidhaa Zimbabwe

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjD

Nchini Zimbabwe,polisi inaendelea kuchukua hatua dhidi ya maduka yanayokwenda kinyume na amri ya serikali,kutopandisha bei za bidhaa.Rais Robert Mugabe,mwezi uliopita alitoa amri kwa maduka yote kusita kupandisha bei za bidhaa.Hatua hiyo imechukuliwa katika juhudi ya kuzuia mfumuko wa bei ambao hivi sasa ni asilimia 4,500.Baada ya kuyalazimisha maduka katika mji mkuu wa Harare na miji mingine kufuata amri hiyo,askaripolisi sasa wameanza kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa amri hiyo inatekelezwa na maduka yalio nje ya miji mikubwa.Kiasi ya wenye maduka 1,800 wamekamatwa kwa madai kuwa wametoza bei za juu kwa bidhaa na huduma zao.Zimbabwe inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula na mafuta ya petroli.Vile vile inakadiriwa kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira ni asilimia 80.