1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Maaskofu wamtaka Mugabe ang´atuke

9 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBG

Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Zimbabwe wamemtaka rais Robert Mugabe amalize ukandamazaji na aondoke madarakani kwa njia ya kidemokrais la sivyo akabiliwe na mapinduzi makubwa.

Baraza la maaskofu nchini humo limesema katika ujumbe wake uliotumwa katika makanisa yote nchini humo kwamba machafuko yamefikia mahala pabaya.

Maaskofu tisa wa kikatoliki wamesema huku Wazimbabwe wakiendelea kuishinikiza serikali kupitia migomo na maandamano serikali inazidi kuwakandamiza kwa kuwakamata, kuwazuilia, kupiga marufuku mikutano ya hadhara, mateso na kuwapiga.

Maelfu ya Wazimbabwe waliokusanyika katika kanisa la mjini Harare kwa misa ya Jumapili, walisukumana kusoma taarifa hiyo iliyobandikwa mahali pa matangazo.

Wazimbabwe wengi akiwemo rais Mugabe ni waumini wa dini ya katoliki.