1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Mataifa magharibi yadai vikwazo zaidi kwa Zimbabwe

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIq

Mataifa ya magharibi yanatowa wito wa kuwekwa kwa vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Zimbabwe kufuatia kushambuliwa kwa wafuasi kadhaa wa upinzani nchini humo.

Serikali ya Zimbabwe imeonya kwamba upinzani utalipa gharama kubwa kwa kile ilichokiita kampeni ya ghasia ya kuianguisha serikali ya nchi hiyo.Waziri wa habari wa Zimbabwe amemshutumu kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai na wanaharakati wengine kwa kuwashambulia polisi wakati wa maandamano dhidi ya serikali yaliopigwa marufuku.

Tsvangirai anapatiwa matibabu hospitalini baada ya yeye na watu wengine 49 kupigwa vibaya na polisi.

Maadamano hayo ya upinzani yalikuwa ni hatua ya karibuni kabisa kupinga sera za Rais Robert Mugabe ambazo zimeitunmbukiza nchi hiyo katika matatizo makubwa kabisa ya kiuchumi.