1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Polisi yakamata zaidi ya wapinzani 200

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxw

Imeripotiwa kwamba polisi ya Zimbabwe imewatia mbaroni zaidi ya wapinzani 200 wakati wakiwa katika mkutano kwenye makao makuu ya chama chao katika mji mkuu wa Harare.

Msemaji wa chama cha upinzani cha Vuguvugu la Mabadiliko ya Demokrasia Nelson Chamisa ameyaambia mashirika ya habari kwamba polisi walioingia katika mkao makuu ya chama hicho walikuwa wameshika bastola na virungu.Amesema kulikuwa hakuna sababu ya kukamatwa kwa wafuasi wao.

Polisi haikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tukio hilo ambalo limekuja miezi miwili baada ya chama cha kiongozi wa chama hicho kikuu cha upinzani cha MDC Morgan Tsvangirai na wafuasi wake kadhaa kutembezewa mkon’goto baada ya kukamatwa na polisi.