1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Iran na Zimbábwe kuunda muungano wa kutetea amani duniani

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMN

Viongozi wa Zimbabwe na Iran wanapanga mkakati wa kuunda muungano utakaopigania amani duniani na kukabiliana na uchokozi wan chi za magharibi.

Serikali ya Zimabwe mjini Harare imethibitisha kwamba Marais Robert Mugabe na Ahmednejad walijadiliana juu ya hatua hiyo kandoni mwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Mkakati huu unajadiliwa baada ya serikali hizo mbili za Zimbabwe na Iran kukosolewa vikali na rais wa Marekani Gorge W Bush hapo jana.Naibu waziri wa habari wa Zimbabwe Bright Matonga amesema Marekani na washirika wake hawapendi kuona amani inatanda duniani.