1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hati ya kukamatwa Al Bashir

15 Julai 2008

Mshtaki wa Mahkama Kuu ya Uhalifu ya kimataifa, Ocampo atoa hati inayoomba kukamatwa kwa rais Al Bashir wa Sudan.

https://p.dw.com/p/Ecnc

Waranati wa kukamatwa rais Omar Al-Bashir wa Sudan si turufu nzito bali ni garasa tu.Hatahivyo, Bashir na wenzake itawapasa kujibu mashtaka ya kuhilikisha umma mkoani Dafur.

Mshtaki mkuu wa Mahkama ya ulimwengu ya kupambana na uhalifu,Luis Moreno-Ocampo,ametega mtego mkali:Ametoa hati ya kuomba kukamatwa Rais wa Sudan Omar Hassan Al-Bashir. Hoja aliyotoa ni kuwa Bashir, ni dhamana kwa mauaji katika mkoa wenye machafuko wa Dafur.Ocampo ametoa ushahidi unaomtia rais huyo wa Sudan hatiani katika kesi 10 mbali mbali za uhalifu wa vita pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu.

Bila shaka, hii ni hatua ya kijasiri aliyochukua Ocampo,lakini haioneshi itaulemaza utawala wa Sudan kama inavyotakiwa .Juu ya hivyo, ni hatua ya kuonesha tu anasakwa kufunfunguliwa mashtaka ambayo ilistahiki zamani kuchukuliwa. Msimamo wa jumuiya kimataifa hadi sasa ukiregarega.

Kuuwawa kwa umma nchini Sudan, kukigonga vichwa vya habari kwa miaka mingi sasa. Ikionesha kana kwamba maafa ya huko hayakuhuzunisha ipasavyo ili kuichukulia Sudan hatua za vikwazo.

Majaribio yote yaliofanywa hadi sasa kukomesha mauaji mkoani Dafur,hayakufika popote.Suluhisho lolote la kisiasa ili kuvikomesha vita huko Dafur,halikuheshimiwa na rais Al-bashir.

Vikwazo vya kiuchumi havikuweza kupitishwa huko Umoja wa Mataifa. Na vipi hatua za kujiingiza kijeshi ? Hazifai kitu,kwani ,China ,inakiuka marufuku ya silaha kwa Sudan na inaiuzia risasi,magari ya kijeshi na hata kutoa mafunzo kwa wanajeshi wake.

Ili kutuma Dafur vikosi vya kuhifadhi amani vya mchanganyiko kati ya UM na Umoja wa Afrika ,Katibu Mkuu Ban Ki-moon alibidi kufunga safari ya omba-omba.

Matokeo yake ni kuwa hadi leo hawajapatikana hata thuluthi-moja ya kikosi kizima cha askari 26,000 kwa Dafur.Kinachotatanisha zaidi hali ya mambo ni kuwa, askari hao kuhifadhi amani kutoka UM hawana mamlaka ya kuwapokonya silaha ama waasi wala wanamgambo wa Janjaweed. Majaribio yote ya kukatisha tamaa yaliofanywa mnamo miaka 5 iliopita ya msukosuko huu hayakufua dafu.....

Jinsi hati ya kudai kutiwa nguvuni rais Al Bashir isivyo na meno makali au au haitafuni, angalia hati zilizotolewa hapo kabla: Mahkama hii ya kimataifa juu ya uhalifu ilitoa waranti wa kukamatwa na kushtakiwa watuhumiwa 2 wa uahlifu wa vita wa Kisudan.Lakini mkono wa Mahkama hiyo ya kimataifa si mrefu vya kutosha.Sudan ikibisha kuwatoa .Badala yake ilimpandisha cheo mtuhumiwa Ahmad Harun na kuwa katibu wa dola anaehusika na maswali ya kiutu.Hilo ni pigo usoni mwa yeyote yule anaetetea haki.

Kwa jicho hilo,hata jaribio hili la sasa la Mahkama hii ya The Hague ,haitawaletea wakaazi wa Dafur nafuu yoyote ya usalama.

Kwani, Sudan, haiitambui Mahkama hiyo na rais Al-Bashir aweza kuendelea kutegemea msaada wa marafiki zake kumtetea:Umoja wa Afrika umeshaonya hatari zinazoweza kuchomoza kwa kumshtaki rais wa Sudan.Na hata China ,hawataachia kutiliwa kitumbnua chao mchanga na kuchafuliwa biashara yao nono na Sudan.