1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya Opel haijulikani bado ?

3 Septemba 2009

General Motors haikuamua bado hatima ya Opel.

https://p.dw.com/p/JOY6
Opel/BochumPicha: picture-alliance/ dpa

Hatima ya tawi la kiwanda cha magari cha General Motors- Opel,bado haijulikani.Kampuni mama nchini Marekani GM linasema mlango uko wazi bado kuhusu nani atalilimiki Opel siku zijazo.

Hali hii imefuatia ripoti ya Jarida la Wall Street Journal kuwa kampuni la General Motors ,linazitaka serikali za Spain,Uingereza na Poland kuchangia Euro Bilioni 1 katika mfuko wa kulijenga upya kampuni la Opel.

"Njia zote zi wazi za kulipatia ufumbuzi kampuni la Ople."

Msemaji wa GM barani Ulaya alisema leo huku uvumi ukienea kwamba ,GM lenye shina lake Detroit,Marekani linazingatia kubakia kulimiliki kampuni la Opel badala ya kuachana na hisa zake kubwa ndani yake na katika lile la Vauxhall,nchini Uingereza.

Likimnukuklu yule lililosema ni afisa wa GM aliehusika katika mazungumzo ,WALL STREET JOURNAL limearifu pia kuwa GM iko tayari kumimina zaidi ya Euro Bilioni 1 ya akiba yake binafsi katika kulijenga upya kampuni la Opel.

Kwa muujibu wa duru za Shirika la habari la Ujerumani DPA, GM ikizingatia mpango huo wa kutia raslimali hiyo endapo tu itashindwa kuuza hisa zake kubwa katika Opel kwa kundi jengine linalotapia kuwa na sauti kubwa ndani yake.

Kurejea shaka shaka mpya juu ya hatima ya kampuni la Opel ,kumezuka wakati huu kuelekea kikao cha Bodi ya GM wiki ijayo kinachotazamiwa kuzingatia mipango ya Opel. Kiasi cha nusu ya wafanyikazi 50.000 wa Opel barani ulaya, wako Ujerumani.

Serikali ya Ujeruman,imeidhinisha ombi la MAGNA -kiwanda cha magari cha Kanada na Austria,la kutaka kununua hisa kubwa ndani ya Opel na serikali kutoa dhamana ya hadi ya Euro bilioni 4.5.

Bodi ya GM lakini,iliamua mwezi uliopita kutopitisha uamuzi juu ya hatima ya Opel huku maafisa wake wakisema wangependa kuiona serikali ya i Berlin inazingatia ombi jengine la tawi lake la ulaya lilitolewa na shirika la RHJ International lenye makao makuu yake Brussels. Kampuni hilo wiki hii ,lilipandisha kima chake hadi hisa 50.1 % kwa Euro milioni 25 hadi kufikia Euro milioni 300 taslim. Serikali ya Ujerumani imejitolea kuipa OPEL mkopo wa Euro bilioni 1.5 kukisaidia kujitoa kwenye msukosuko wake wa sasa.

Mazungumzo juu ya hatima ya kiwanda cha Opel,yamekuja wakati mbaya kwa Kanzela Angela Merkel,wiki chache tu kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu .

Mwandishi:Ramadhan Ali/DAPE

Mhariri:M.Abdul-Rahman