1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye Marekani yaridhia mkataba

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cc36

BALI.Hatimaye viongozi wa dunia wamefikia muafaka katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuanisha njia za kuelekea kwenye mkataba mpya wa kupambana na ogezeko la ujoto duniani.

Baada ya saa kadhaa za majadiliano, katika siku ya mwisho wa mkutano huo huko Bali Indonesia, karibu mataifa yote 190 yaliridhia njia ya kuelekea katika mkataba huo ifikapo mwaka 2009.

Muafaka huo ulifikiwa baada ya Marekani kuamua kuondoa upinzani wake na kukubali kama ilivyopendekezwa na nchi nyingine zilizoendelea.

Mkataba huo mpya unategemewa kuchukua nafasi ya ule wa Kyoto unaomalizika mwaka 2012.

Mapema Marekani na Umoja wa Ulaya walikubaliana kuwa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani katika wakati huu kuelekea mkataba huo mpya hazijikita zaidi na upungazaji wa gesi inayoharibu mazingira.