1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Urusi Capello katika hali ngumu

15 Juni 2015

Makocha Fabio Capello na Guus Hiddink wako katika hali ngumu kuhusiana na hatma yao wakati timu zao Uholanzi na Urusi, zikipambana kufuzu katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2016

https://p.dw.com/p/1FhXo
Interaktiver WM-Check 2014 Trainer Russland Capello
Picha: Kirill Kudryavtsev/AFP/Getty Images

Shirikisho la kandanda la Urusi linatafakari hatma ya Capello mwenye umri wa miaka 68 baada ya kichapo cha bao moja kwa sifuri dhidi ya viongozi wa Kundi G Austria na kuwaacha katika nafasi ya tatu pointi nne nyuma ya nambari mbili Sweden.

Uholanzi iliishinda Latvia magoli mawili kwa moja wakati England ikiifunga Slovania mabao matatu kwa mawili. Katika matokeo mengine ya mechi za jana Sweden iliifunga Montenegro mabao 3-1. Uhispania ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Belarus nayo Uswisi ikaibwaga Lithuania kwa mabao 2-1. Ukraine iliangusha Luxembourg mabao 3-0.

Katika michezo ya Jumamosi Ujerumani iliiangamiza Gilbratar kwa kuitandika magoli 7-0 nayo Poland ikailaza Georgia mabao 4-0. Scotland na Jamhuri ya Ireland zitoka sare ya bao 1-1.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga