1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatua ya mwisho ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya

Sekione Kitojo
26 Mei 2019

Vituo vya kupigia kura katika mataifa 21 ya Umoja wa Ulaya vimefunguliwa, mataifa saba tayari yamekwisha piga kura. Mara baada ya kura kuhesabiwa, bunge  jipya la Umoja huo linatarajiwa kuelekea upande wa kulia.

https://p.dw.com/p/3J5aD
Schweden Stockholm Parlamentswahl
Picha: Getty Images/AFP/J. Nackstrand

Vituo vya  kupigia  kura vitafunguliwa  katika  mataifa  21 Jumapili (26.05.2019), ikiwa  ni  pamoja  na  mataifa makubwa  ya  Umoja  wa  Ulaya ya  Ujerumani, Ufaransa, Italia, Uhispania na  Poland.

Schweden Stockholm Parlamentswahl
Wapiga kura wakipiga kura zao katika uchaguzi wa bunge la UlayaPicha: Getty Images/AFP/J. Nackstrand

Mataifa  haya  matano kwa pamoja yanatoa  karibu  nusu  ya  wabunge  wa Umoja  wa  Ulaya  katika  bunge  hilo,348 kutoka  idadi ya wabunge 751.

Upigaji  kura  katika  bunge pekee  la  kimataifa  duniani ulianza  siku ya Alhamis  ambapo Uholanzi  na  Uingereza  zilianza kupiga  kura , na  kisha kufuatiwa  na  Ireland  na  Jamhuri  ya  Cheki siku  ya  Ijumaa  na  Latvia, Malta na  Slovakia siku ya  Jumamosi.

Jumla  ya  raia  milioni 420 wanahaki  ya  kupiga  kura . Watafiti wa  uchaguzi wanatarajia kiwango  cha  chini  cha wapiga  kura  katika  uchaguzi  wa  hapo awali  mwaka  2014, ambao  ilikuwa  ni  asilimia  43  tu, inaweza  kupanda kidogo  mara  hii.

Vyama  vikubwa vya  kisiasa  katika  Umoja  wa  Ulaya  vimesema  uchaguzi wa  mwaka  huu  unaweza  kuwa  uchaguzi  wa  mabdiliko  katika  maisha.

Wagombea wakuu  katika chama  cha siasa za wastani za  mrengo wa  kulia cha  European  Peoples Party EPP, Manfred Weber  wa  Ujerumani, na mgombea wa  chama  cha  siasa  za  wastani  za  mrengo wa  kushoto kwa upande wa  wasoshalisti barani  Ulaya, Frans Timmermans, PES, makamu wa  rais wa  halmashauri ya  Umoja  wa  Ulaya  anayeondoka  madarakani kutoka  Uholanzi, wote wanakubaliana  kuhusiana  na maelezo  haya wakati wa  kampeni  za  uchaguzi.

Deutschland | One Europe for all-Demo in Frankfurt a. M.
Waandamanaji wakishiriki katika maandanao ya "Ulaya moja kwa wote" mjini Frankfurt Mei 19, 2019Picha: Getty Images/T. Lohnes

Ulinzi wa maadili ya kidemokrasia

Wasi  wasi  wao  mkubwa  katika  uchaguzi  huu  ni kuendelea  na  hali  ya umoja  katika  Umoja  wa  Ulaya, kulinda demokrasia  ya  "kiliberali" utaratibu unaooungwa  mkono  na  vyama vya  sisa  za  kizalendo miongoni  mwa waziri  mkuu  wa  Hungary Viktor Orban.

Mwanasiasa  wa  Italia  mfuasi  wa  siasa  kali za  mrengo wa  kulia  Matteo Salvini , kwa  upande wake, anataka  kupunguza  kwa  kiasi  kikubwa ushirikiano  na  Umoja  wa  Ulaya.

Kama  walivyo wafuasi wa  siasa  za  kizalendo  katika  mataifa  wanachama wa  Umoja  wa  Ulaya, Salvini  anafuata  kauli  mbiu ya "Nchi yangu  kwanza" chama  chake  huenda  kikawa  nguvu  ya  ushawishi nchini  Italia  katika uchaguzi  huu.

Wiki ya  mwisho ya kuelekea  katika  uchaguzi  huu  bila  shaka  haikukosa vituko. Nchini  Austria, muungano wa  kihafidhina unaounda  serikali uliporomoka  baada  ya  mwanachama  wa  chama  cha  siasa  kali  za mrengo  wa  kulia  cha  Freedom  Party, kiongozi wa  zamani  Heinz-Christian Strache, alionekana  katika  vidio  akionekana  kutoa kandarasi ya  serikali kwa  mpwa wa tajiri  mkubwa  wa  Urusi  ili  kuweza  kupata  msaada  wa kampeni.

Deutschland | One Europe for all-Demo in Frankfurt a. M.
Maandamano ya "Ulaya moja kwa wote" mjini FrankfurtPicha: Getty Images/T. Lohnes

Wachunguzi  wa  uchaguzi  bado  wana  shaka  iwapo kashfa hii  itakuwa  na athari  yoyote katika  uchaguzi wa  Umoja  wa  Ulaya.

Davide Ferrari , wa taasisi ya  utafiti  ya  Votewatch  mjini  Brussels, ameiambia  DW kwamba  athari  zitakuwa  ndogo kwa  Austria. Wapiga  kura wa  siasa  kali  za  kizalendo  hawajali  kabisa  kuhusu maadili. Kwa  wao ni kuhusiana  na  upinzani tu," amesema.

Mwandishi: Bernd Riegert / Brussels / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Yusra Buwayhid