1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA:Castro aonekana katika runinga akiwa na afya nzuri

31 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWK

Television ya Cuba, imemuonesha kiongozi anayeumwa wa nchi hiyo Fidel Castro akizungumza na Rais wa Venezuela Hugo Chavez ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitatu.

Castro alionekana akiwa na hali nzuri tofauti na alivyoonekana katika picha za mara ya kwanza.

Kiongozi huyo wa Cuba mwenye umri wa miaka 80 alifanyiwa upasuaji kutokana na kuvuja damu tumboni na alikabidhi kwa muda madaraka ya uongozi kwa mdogo wake Raul.

Hugo Charvez ni mfuasi mkubwa wa Castro.