1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM: Mkutano kujadili mgogoro wa Darfur

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtn

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa,amewaalika mawaziri wa nje wa mataifa makuu,kuhudhuria mkutano utakaofanywa tarehe 25 mwezi Juni kujadili mgogoro wa jimbo la Darfur,lililokumbwa na vita magharibi ya Sudan.Mkutano huo pia utahudhuriwa na China inayokosolewa na jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya msimamo wake kuhusu Darfur.Sarkozy alipozungumza pembezoni mwa mkutano wa G-8 unaofanywa Heiligendamm,nchini Ujerumani alisema,madola makuu yanataka kuchukua hatua kwa haraka ili kukomesha mgogoro ulioua hadi watu 200,000 katika jimbo la Darfur.Marekani nayo katika Umoja wa Mataifa,ilikariri onyo lake kuitaka Sudan ikubaliane na pendekezo la Umoja wa Mataifala kutaka kupeleka Darfur,vikosi vya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.