1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HERAT:Shambulio la marekani laua raia 40 Afghanstan

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5H

Uchunguzi uliofanywa na maofisa wa Afghanstan umegundua kuwa kiasi cha raia 40 wengi wakiwa ni wanawake na watoto waliuwawa katika opresheni ya kijeshi ya hivi karibuni iliyoongozwa na wanajeshi wa Marekani katika mkoa wa magharibi wa Herat.

Maofisa wa Kijeshi wa Marekani walidai wanajeshi wao waliwauwa zaidi ya washukiwa 140 wa kundi la Taliban katika opresheni mbili tofauti.

Rais Hamid Karzai wa Afghanstan amesema kitendo cha kuuwawa kwa raia hakikubaliki na amewatolea mwito wanajeshi kutafuta njia za kuepuka mauaji hayo ya raia.