1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HIROSHIMA : Abe asakama matumizi ya bomu la nuklea

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbd

Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe ameapa kuendeleza juhudi za kupiga marufuku silaha za nuklea wakati mji wa Hiroshima ukiwa na kumbukumbu ya miaka 62 ya shambulio la kwanza la bomu la nuklea duniani.

Watu 45,000 leo wamebaki kimya kwa dakika moja kukumbuka wakati hasa bomu hilo lilipodondoshwa katika mji wa Hiroshima hapo tarehe 6 mwezi wa Augusti mwaka 1945 na kuuwa zaidi ya watu 140,000.

Maelfu kwa maelfu ya watu wengine waliathirika vibaya kutokana na miale ya sumu za uklea au kutokana na kuunguwa.

Tokea wakati huo kutoka na kushindwa katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Japani imekuwa rasmi ni nchi yenye kupiga vita.