1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Historia ya all-Africa Games

Ramadhan Ali11 Julai 2007

Michezo ya 9 ya bara la Afrika-all.Africa Games imefunguliwa jana mjini Algiers huku wanariadha takriban wa bara zima wakishiriki.Kinyan'ganyiro cha medali na msisimko kitatuwama katika riadha.humo majogoo wa Kenya,ethiopia,Morocco na wenyeji Algeria watatia fora.

https://p.dw.com/p/CHbk

Michezo ya 9 ya bara la Afrika-All-Africa Games ilifunguliwa jana rasmi mjini Algiers kwa shangwe na shamra shamra ikihudhuriwa na takriban na wanariadha wake kwa waume kutoka nchi zote 53 za Afrika.Hii ni tofauti kabisa na michezo ya kwanza 1965 mjini Brazzaville,Kongo, pale nchi 16 tu huru za Afrika ziliposhiriki.

Michezo ya ni ya pili kufanyika Algiers,kwani Algeria,iliandaa ile ya 3, 1978 kabla Nairobi,kuandaa michezo ya 4 na ya kwanza kwa Afrika Mashariki hapo 1987.

Michezo ya kwanza ya bara la Afrika asili yake ilikua ifanyike Alexandria,Misri lakini dola za kikoloni zikaitia munda dakika ya mwisho ili kuzuwia maingiliano ya watu wa makoloni yao.Kama michezo ya olimpik ya kisasa-moder Olympic games-raia ya kuandaa michezo ya bara la Afrika ilitokana na mfaransa Pierre de Coubertin.

Baada ya kutiwa munda michezo iliokua ifanyike Alexandria,ilichukua muda hadi 1965 mjini Brazzaville,Kongo kwa wanariadha wake kwa waume kupimana nguvu katika medani ya spoti.

Mafanikio huko Brazzaville ya wanariadha wa Kenya,Nigeria,Ghana,Senegal na Uganda yalijenga msingi wa nguvu za riadha za Afrika za hii leo.Kwani, leo hakuna mashindano yoyote ya riadha yanayokamilika bila ya majogoo wa Afrika.

Michezo ya Brazzaville kisiasa pia ilikua ndio hatua kubwa kabisa barani afrika tangu kispoti au vbyenginevyo kuwaunganisha vijana wa Afrika.

Kwani, kwa mara ya kwsanza kabisa ilionekana waafrika wa asili mbali mbali-magharibi-mashariki na kaskazini wakijumuika pamoja chini ya bendera ya spoti.

Michezo ya 2 ya bara la Afrika-2nd-All-Africa Games,Januari,1973 ilifanyika Lagos,Nigeria,miezi 3 tu baada ya michezo ya olimpik ya Munich,1972.Kuhudhuria huko Lagos kwa majogoo wa Afrika mashuhuri ulimwenguni na mabingwa wa Olimpik kama Kip Keino na Ben Jipcho wa Kenya;John Akii-bua wa Uganda,Miruz Yifter na Mamo Wolde wa Ethiopia pamoja na Philbert bayi wa Tanzania kulichemsha hamasa na hisia katika michezo ile.Kwani,Lagos, iliwapa mashabiki wa Afrika nafasi nadra ya kuwaona mabingwa wao-akina Kip Keino,Ben jipcho na Akii-bua waliotamba katika michezo ya Olimpik ya Munich.

Miongoni mwa chipukizi wapya waliogonga vichwa vya habari huko Lagos alikua Mtanzania Philbert Bayi.Kwani alikua Bayi,aliethubutu kumvua taji Kip Keino kama mfalme wa mbio za mita 1500 alipomshinda kumfungisha virago kwenda New York kujiunga na shirika la ITA la wanariadha waajiriwa-professional Track.

Jogoo mwengine aliewika Lagos,alikua Benjamin Jipcho “The Big Ben”.Jipcho n die aliekua hnasa arudi Nairobi na medali ya dhahabu ya olimpik kutoka mita 3000 kuruka viunzi.

Lakini, wapi,Kip keino alitoroka nayo na hivyo iliobakia kwa Jipcho ni kuubainishia ulimwengu mjini Lagos kwamba ni yeye ndie bingwa wa wote alipoweka rekodi ya kwanza ya dunia katika ardhi ya Afrika:Muda wake ulikuwa dakika 8,sek.20.8.

Kwa michezo ya 3 ya bara la Afrika ,wanariadha kutoka mataifa 45 ya afrika huru waliwasili Algiers,Algeria,kituo cha michezo ya hivi sasa.Kuanzia Julai 13-28,1978.huko wakenya na wanigeria walionesha uhasayma wsao-wakenya wakitamba katika mbio za masafa ya kati na marefu wakati wanigeria katika masafa mafupi-sprints.

Katika mita 3000 kuruka viunzi,Henry Rono aliowaongoza wakenya wenzake 2 kunyakua nafasi ya kwanza nay a pili kabla yeye mwenyewe kuja kuweka rekodi 4 za dunia mnamo muda wa siku 80.

Kwa michezo ya 4,Afrika ilibidi kusubiri kitambo kirefu-miaka 9 pale Nairobi,Kenya ilipoandaa michezo ya kwanza na pekee ya bara la Afrika kwa afrika mashariki.

Baada ya ile ya Algiers,1978,michezo ya Nairobi ilikua ndio michezo mikubwa kabisa ya kispoti barani humo kuandaliwa katika bara la afrika.Jumla ya nchi 41 ziliwasili na vikosi tofauti ili kutamba huko kasarani.Visiwa vya bahari ya hindi kama Mauritius na Seyschelles havikuziachia uwanja pekee dola kuu za spoti Misri,Nigeria na Kenya.

Kenya ilikaribisha nchi 12 zaidi kuliko Algiers.Idadi ya wanariadha 6000 walishiriki Nairobi wakishiriki katika zaidi ya michezo darzeni 1.Uwanja wa kisasa wa Kasarani na wa Nyayo ukanyanyua juu rekodi za Afrika.

Kuanzia jana kizazi kipya cha wanariadha wa Afrika-wake kwa waume kinafuata nyayo za akina Kip Keino na mamo wolde waliotamba Brazzaville,1965.Algiers, 2007 inawanoa wanariadha wa Afrika kwa mashindano ya mwezi ujao ya ubingwa wa dunia huko Osaka,Japan,lakini pia kiyoo cha kumurika nguvu za riadha za Afrika kwa michezo ya mwakani ya olimpik,mjini Beijing.