1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Historia ya mashindano ya riadha ulimwenguni

11 Agosti 2009

World Athletics championship Berlin jumamosi:

https://p.dw.com/p/J7qF
Asafa Powell, na UsainPicha: AP

Kila baada ya miaka 2, mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni-world Athletics Championship hufanyika.Baada ya yale ya Osaka,Japan, miaka 2 iliopita, wanariadha wake kwa waume kutoka mabara yote, watapimana nguvu kuanzia jumamosi hiii ijayo August 15-23 mjini Berlin,Ujerumani.

hii ni historia ya mashindano haya chini ya paa la International Amatuer Athletics Federation (IAAF) na lini hasa yalianza ?:

Yalipofanyika kwa mara ya kwanza 1983 mjini Helsinki, Finland, wanariadha mashuhuri waliogonga vichwa vya habari hawakuwa kutoka bara la afrika-kinyume na mashindano ya baadae:Chipukizi wa Marekani wakati ule Carl Lewis,alieazimia kufuata nyayo za marehemu Jesse Owens,kipenzi cha michezo ya olimpik ya Berlin,1936 alipoweka rekodi 4 katika mbio za kasi ndie aliegonga vichwa vya habari kabla kupiga mhuri wake katiika michezo ya olimpik ya Los Angeles,mwaka mmoja baadae.

Mwengine, alikuwa Sergei bubka wa Ukraine-bingwa wa rekodi kadhaa katika pole-vault au kuruka juu kwa upongoo.

Asiilii ya mashindano haya ya riadha-ambayo ndio moyo na msisimko wa michezo yoyote ya olimpik, ilikuwa 1976-mwaka wsa michezo ya Olimpik ya Montreal,iliosusiwa na sehemu kubwa ya nchi za kiafrika kwa ajili ya New Zealand.

Ndio kulikuwapo mashindano ya riadha kwa bara la ulaya na ya bara la afrika-all Africa Games,yalioasisiwa Brazzaville, 1975 ingawa yalijumuisha michezo mengine.Wanariadha wa dunia walitaka mashindano yao pekee ya kupimana nguvu nje ya Olimpik.Hivyo, 1983 wanariadha 1,355 kutoka mataifa 154 walikutana mjini Helsinki,mji wa mwanariadha maarufu wa miaka ya 1920 Paavo nurmi kwa mashindano yao ya kwanza kabisa kati ya august 7-14.

Miongoni mwa mabingwa wa kwanza wa mashindano ya helsinki alikuwa msiichana wa Ujerumani Mashariki Marlies Goehr alietamba katika mita 100,Jarmila Kratochvilova wa Jamhuri ya Czech katika masafa ya mita 400 na car Lewis aliewika katika mita 100, mita 100x4 kupokezana na Long jum akifuata nyayo za jesse Oqwens Berlin, 1936.

Tangu enzi za Helsinki ambako Said Aouita wa Morocco,aliwasilii kwa mara ya kwanza katika medani ya riadha kabla hakuanza kutia fora katika mta 5000,mashindano haya yamekuwa hadi wanariadha 1,978 mwaka 2003 yalipofanyika yale ya Osaka,Japan 2003.

Mashindano 8 ya ubiingwa wa dunia tayari yamefanyika ulaya na Japan imeyaandaa mara 2-mbali na Osaka mwaka 2007 ,jiji la Tokyo liliandaa 1991.Mji wa Edmonton,Kanada, uliyakaribisha 2001. Dola kuu la riadha ulimwenguni, marekanii bado kuandaa world athletics championshiip.Hii ni mara ya pili kwa mashindano haya kuja Ujerumani baada ya yale ya Stuttgart 2003 alipotia fora kwa mara ya kwanza mzee Haile Gebrselassiie wa Ethiopia.Berlin,2009 atatia fora muethiopia mwengine - Bekele upande wa wanaume na Turnesh Dibaba ule wa wasichana.

Mashindano ya Stuttgart nakumbuka yalinawirishwa na mrembo wa jamaica Merlen Ottey alipompita ufondoni na picha kubidi kuamua mshindi Gail Devers wa Marekani katika changamoto ya mita 100.Ben johnson wa Kanada alipoteza taji lake la mita 100 na rekodi yake ya dunia ya 1987 alipokashifiwa na kutimuliwa nje ya kijiji cha olimpik cha seoul, 1988.

Mashiindano ya 12 ya ubingwa wa dunia Berlin,jumamosi hii yanasubiri msisimko mwengine mkubwa katika mbio za kasi za mita 100 na 200 kati ya mjamaica.

Mwandishi: Ramadhan Ali

Mhariri:Abdul-Rahman