1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ho Chi Minh City. Kimbunga chaharibu nyumba na maboti.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmC

Kimbunga kinachojulikana kama Durian kimelikumba eneo la kusini mwa Vietnam , na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na kuharibu nyumba na maboti.

Kimbunga hicho , ambacho kilikuwa na upepo wenye kasi ya zaidi ya kilometa 120 kwa saa , kililikumba eneo la bonde la jimbo la Mekong na kisiwa cha Phu Quy.

Katika sehemu kilimopitia , Durian kimesababisha watu 1,300 kufariki ama wamepotea nchini Philipines, ambako kilishambulia kwanza wiki iliyopita.

Mvua zilisababisha maporomoko ya matope ambayo yamefunika vijiji kadha karibu na mlima Mayon.

Rais wa Philippines Gloria macapagal Arroyo ametembelea eneo hilo la maafa . Ndege mbili za mizogo za Indonesia zimepeleka chakula na madawa nchini humo.

Wavuvi wa Hispania wameweka hospitali ya muda kwa watu walionusurika ambao wamejeruhiwa.