1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hong Kong chini ya kiwingu cha sheria mpya ya usalama

Tatu Karema
7 Julai 2020

China imezindua nguvu mpya ya kuthibiti uwezo wa kupata huduma za intaneti mjini Hong Kong kwa kutumia sheria yake mpya ya usalama wa kitaifa lakini kampuni kubwa za teknologia za Marekani zimeibua upinzani

https://p.dw.com/p/3eu7B
Hongkong Sicherheitsgesetz Carrie Lam
Picha: Getty Images/AFP/I. Lawrence

Kampuni kubwa za teknologia za Facebook, Google na twitter, zilisema jana kuwa zimekataa maombi  ya serikali ya Hong Kong ama idara ya polisi ya kutoa habari kuhusu watumiaji wa mitandao hiyo.

Katika taarifa, kampuni inayomiliki mtandao wa Facebook na huduma yake maarufu ya kutuma ujumbe ya WhatsApp zimekataa maombi hayo hadi itakapofanya tathmini ya sheria hiyo ambayo inahusu uangalifu kamili wa haki rasmi za binadamu na mashauriano na wataalamu wa haki za binadamu. Mipango hiyo ya kudhibiti shughuli za intaneti ilijumuishwa  katika nyaraka ya serikali ya kurasa 116 iliyotolewa jana usiku.

Licha ya hakikisho kwamba ni watu wachache watakaolengwa na sheria hiyo, maelezo mapya yanaonesha kuwa haya ndio mabadiliko makali zaidi katika haki na uhuru wa Hong Kong tangu eneo hilo kukabidhiwa serikali ya China kutoka Uingereza mwaka 1997.

Pompeo akashifu kuhusu hatua za kiholela dhidi ya wakazi wa Hong Kong

Hapo jana jioni, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, alikashifu hatua za kiholela za kuwadhibiti wanaharakati, shule na maktaba tangu sheria hiyo ilipoidhinishwa. Wakati huo huo, Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amesema leo kwamba kamati mpya ya usalama wa kitaifa iliyoundwa hivi majuzi itafanya shughuli zake kwa njia ya siri kulinda usalama wa kitaifa chini ya sheria mpya iliyowekewa eneo hilo na serikali ya China wiki iliyopita.

Wakati wa kikao na wanahabari hii leo, Lam alishindwa kutoa hakikisho kwa wanahabari hao baada ya wasiwasi kuibuliwa kuhusu kutokuwa na uwazi wa makosa yanayohusiana na vyombo vya habari.Lam aliongeza kuwa hatimaye , wakati na ukweli utadhihirisha kwamba sheria hiyo haitahujumu haki na uhuru wa kibinadamun na kwamba sheria hiyo itadumisha udhibiti kwa Hong Kong. Ames Sheria hii itahakikisha kwamba sera hii muhimu ya nchi moja mifumo miwili inaweza kuendelea na Hong Kong kufurahia udhibiti na ufanisi wa muda mrefu.

Maelezo ya kutumiwa kwa sheria hiyo yalitolewa jana jioni na kuipa idara ya polisi nguvu zaidi chini ya sheria hiyo ya usalama wa kitaifa inayojumuisha uwezo wa kukamata vifaa vya elektroniki, kuingia katika majengo bila vibali, kufungia mali na kuthibiti matembezi ya watu. China iliweka sheria hiyo mpya kulenga kupingwa kwa mamlaka, hali ya kutaka kujitenga, ugaidi na kushirikiana na vikosi vya kigeni.