1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HONIARA: Watu sita wauwawa kwenye tsunami

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCD9

Tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 8.0 katika kipimo cha Richter limetokea katika eneo la kusini mwa bahari ya Pacific na kusababisha tsunami katika visiwa vya Solomon.

Msemaji wa serikali visiwani humo, George Herming, amethibitisha katika taarifa aliyoitoa kwamba watu wasiopungua sita wameuwawa, lakini akasisitiza idadi ya vifo huenda kuongezeka.

Msemaji huyo amesema vijiji, shule na vituo vya afya vimeharibiwa na mawimbi makubwa ya tsunami. Visiwa vya Gizo, Lefung na Taro vimeathiriwa zaidi na mawimbi hayo ya tsunami.

Tatizo la mawasiliano nchini humo, iliyo na visiwa na karibu 1,000, linaifanya kazi ya kutathmini uharibifu uliosababishwa na tsunami hiyo kuwa ngumu.

Mfumo wa kuonya juu ya kutokea tsumani katika eneo la bahari ya Pacific umeondolewa.