1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hosni Mubarak ashinikizwa ajiuzulu

Thelma Mwadzaya26 Januari 2011

Watu wawili na afisa mmoja wa polisi wameuawa nchini Misri kwenye maandamano ya kumshinikiza Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.

https://p.dw.com/p/103DX
Waandamanaji mjini Cairo,MisriPicha: AP

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama aliyeko kwenye mji wa bandari wa Suez,waandamanaji hao waliuawa pale ghasia zilipozozuka katika yao na maafisa wa polisi.Afisa  huyo mmoja wa polisi aliuawa baada ya kujeruhiwa katikati ya mji mkuu wa Misri wa Cairo,kulikofanyika maandamano ya kumtaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.Kulingana na kiongozi  wa kundi la Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku,Gamal Heshmat,raia hawana imani na uongozi uliopo.

NO FLASH Ägypten Kairo Proteste Mubarak Polizei Demonstration
Waandamanaji wanaomshinikiza Hosni Mubaraka ajiuzulu:polisi wa ghasia chonjoPicha: AP

Mwanasiasa huyo wa upinzani alisisitiza kuwa ijapokuwa serikali imeahidi itafanya mageuzi,hatua bora ni kujizulu.  

Polisi wa kupambana na ghasia walilazimika kuwafyatulia mabomu ya gesi ya machozi maelfu ya waandamanaji ambao wengi wao ni vijana waliorusha mawe na kupiga mayowe.