1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar

23 Novemba 2009

Chama kikuu cha upinzani Visiwani Zanzibar cha CUF kimempongeza Rais wa visiwa hivyo Amani Abeid Karume kwa hotuba yake hapo jana kutangaza rasmi kuzikwa kwa uhasama wa kisiasa uliyokuwepo baina ya vyama hivyo viwili.

https://p.dw.com/p/KdVo
Rais Amani Karume wa ZanzibarPicha: AP Photo

Rais Karume alitoa hotuba hiyo katika mkutano wa hadhara siku chache tu baada ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad kutangaza kuwa chama chake kumemtambua rasmi Rais Karume, kufuatia mkutano wa faragha kati ya viongozi hao wawili.

Akizungumza na mwenzangu Aboubakary Liongo, Mkuu wa idara ya nje na uhusiano wa kimataifa wa chama hicho cha CUF, Ismail Jussa alisema hotuba hiyo ya Rais Karume imedhihirisha nia aliyokuwa nayo ya kuiona Zanzibar inakuwa salama na amani.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman