1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Mashambulizi yasababisha vifo vya watu wengi Tigray

Tatu Karema
11 Februari 2021

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la HRW limesema wanajeshi wa Ethiopia walitumia wiki za mwanzo za mzozo wa jimbo la Tigray kuyashambulia kwa silaha nzito maeneo yenye watu wengi na kusababisha vifo vya raia 83.

https://p.dw.com/p/3pDQ1
Äthiopien I  Sudan I Konflik
Picha: Nariman El-Mofty/AP/picture-alliance

Kulingana na ripoti ya shirika hilo vikosi vya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed vilizilenga nyumba za makaazi, hospitali, shule na masoko katika maeneo ya mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele na miji mingine ya Shire na Humera. Human Rights Watch imeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza iwapo sheria za vita zilikiukwa kutokana na taarifa kwamba wanajeshi walifanya mshambulizi bila kubagua na kusababsiha vifo vya watu na kuharibu mali. Operesheni ya kijeshi dhidi ya jimbo la Tigray ilitangazwa Novemba mwaka uliopita na Waziri Mkuu Abiy aliyewatuhumu viongozi wa chama cha TPLF kilichokuwa kinaongoza eneo hilo kwa uhaini baada ya kuzishambulia kambi za jeshi la taifa.