1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda dhahabu kaskazini mwa Mali ikawanufaisha magaidi

Amina Mjahid
14 Februari 2020

Kumeibuka wasiwasi katika eneo moja la kaskazini mwa Mali ambako wanamgambo wanaohusishwa na kundi la al-Qaida wana makao yao, baada ya uvumbuzi wa dhahabu katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/3XlzL
Goldsuche in Mali
Picha: picture-alliance/Valeriy Melnikov/RIA Novosti

Kuna hofu kwamba huenda madini hayo yakaunufaisha sio tu uchumi wa eneo hilo bali hata wanamgambo wa Kiislamu.

Muungano wa waasi wa Tuareg wanaojulikana kama CMA wanalidhibiti eneo la Kidal na viongozi wake ndio wanaosimamia mpango huo wa dhahabu.

Baadhi ya wanachama wa CMA wanaaminika kuwa na mahusiano ya karibu na kundi la JNIM ambalo ni mshirika wa al-Qaida katika eneo hilo.

Maafisa wa CMA wamekataa kuzungumzia uwepo wa wapiganaji walio na uhusiano na al-Qaida miongoni mwao.

Wakaazi pia wanahofia kuzungumzia suala hilo wakisema kundi hilo la magaidi lina maafisa wa kijasusi katika kila sehemu mjini humo.