1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu dhidi ya mzee Fritzl kutolewa leo

19 Machi 2009

Mahakama ya St Pöelten imeshasikiliza ushahidi wa binti ya mzee Fritzl,uliomfanya mzee huyo ghafla kukiri makosa yote yanayomkabili

https://p.dw.com/p/HFBm
''Josef Fritzl,katikati akisindikizwa na polisi baada ya kikao cha pili cha kesi dhidi yake.''Picha: AP

Mahakama ya mjini St Pöelten nchini Austria leo inatazamiwa kutoa hukumu yake dhidi ya mtuhumiwa bwana Fritzl aliyekiri mashataka yote yanayomkabili katika kesi ya kumzuia mateka bintiyake kwa miaka 24,kumbaka na kumzalisha watoto saba.

Awali mtu huyo mwenye umri wa miaka 73 kwa jina la Josef Fritzl alikubali kutenda makosa ya kuzaa na mwanawe kwa nguvu,na kumbaka lakini akakanusha mashataka mengine ya kuua na kumfanya mtumwa mwanawe huyo wa kike.

Mtu huyo anadaiwa kusababisha kifo cha mwanawe mchanga aliyemzaa na bintiyake baada ya kushindwa kutafuta huduma za matibabu kwa ajili ya mtoto huyo aliyefariki mwaka 1996.

Hatua ya bwana Fritzl ya kukiri makosa yote ilikuja baada ya mahakama kuutazama kwa saa kadhaa ukanda wa video wa bintiyake akitoa ushahidi.

Mzee huyo akikutwa na hatia ya kutenda makosa yote hayo huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Saumu Mwasimba/ZR