1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya mauaji Dresden

Sekione Kitojo12 Novemba 2009

Katika kesi ya kuuwawa kwa Marwa EL-Sherbini, mshtakiwa Alex W. amehukumiwa kifungo cha maisha, katika hukumu ambayo imechukua msimamo thabit.

https://p.dw.com/p/KUaq
Waislamu wakisali na wengine walifanya maandamano siku ya Jumatano wakati wa kutolewa hukumu mjini Dresden.Picha: AP

Katika kesi ya kuuwawa kwa Marwa El-Sherbini , mshtakiwa Alex W. amehukumiwa kifungo cha maisha. Ni hukumu iliyochukua msimamo thabit.

Wajerumani wengi kwa upande wao wanaliona tukio hilo la mauaji kuwa ni tukio lililofanywa na mtu ambaye ana msimamo mkali. Wanashangaa kuona hisia kali zinazoonyeshwa na Waislamu na wanaona kuwa wanaonyesha hisia za kupita kiasi na kwamba hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Mahakama haikuchukua hata hivyo uamuzi huu kutokana na kiwango cha hisia zilizoonyeshwa ama kiwango cha chuki dhidi ya Uislamu inayopatikana katika jamii ya Wajerumani.

Ilikuwa hukumu ambayo imeangalia suala la mauaji na sababu zake. Na hukumu hii imepitishwa kwa uhalali kabisa. Tukio la mauaji linachukua adhabu kali . Mtu huyo atakuwa kifungoni maisha na suala la kuachiliwa baada ya muda fulani halipo.

Kwa hukumu hii mahakama kimsingi imejiwekea hadhi ya kuaminika. Watu wenye msimamo wa chuki dhidi ya wageni ama hata kufanya mauaji dhidi yao nchini Ujerumani hawatavumiliwa.

Watakabiliwa na adhabu ya juu kabisa kisheria. Mambo mawili hata hivyo hayajafafanuliwa. Kwanza kwa Waislamu wengi , haiingii akilini , kwamba katika nchi yenye usalama kama Ujerumani , muuaji anaweza kuingia na kisu mahakamani. Kwa wengine , katika hali tofauti mauaji haya yanamfanya Muislamu na asiye Muislamu kufikia hali ya kutafakari zaidi.

Kwa bahati hakukuwa na matukio ya ghasia na kufikisha hali mbaya ya kutofahamiana, kama iliyotokea katika mwaka 2006 ambapo kulikuwa na mzozo wa kashfa ya katuni na baadaye mvutano kuhusiana na matamshi ya Pope Benedict mjini Regensburg nchini Ujerumani.

Kwa bahati mbaya kwa upande wa Waislamu hakukuwa na kauli za kutosha , ambazo zinaeleza wazi kuwa nchini Ujerumani Waislamu hawabaguliwi na serikali ama kufanyiwa fujo na matumizi ya nguvu. Na kwa bahati mbaya kwa upande wa Ujerumani pia hakuna kauli za kutosha zinazofafanua na kutambua undani wa tatizo hili. Maoni ya watu yanasema kuwa , xsehemu moja ya jamii ya Wajerumani inawasi wasi mkubwa, hawawaamini na pia kuna hali ya wazi ya uadui dhidi ya Uislamu. Kwa hiyo jamii ya Wajerumani inapaswa kujadili pamoja na Waislamu kuhusiana na mfumo unaostahiki wa imani ya Uislamu.

Mwandishi: Sollich,Rainer/ZR/Sekione Kitojo

Mhariri:M.Abdul-Rahman