1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya kifo yapungua Afrika

12 Aprili 2018

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema visa vya hukumu ya kifo vimepungua katika mataifa yaliyo chini ya Jangwa la Sahara.

https://p.dw.com/p/2vu8g
Japan Protest gegen die Todesstrafe
Picha: Getty Images/AFP/Y. Tsuno

Mataifa yaliyo chini ya Jangwa la Sahara yamepiga hatua kubwa ya vita dhidi ya hukumu ya kifo. Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty linasema kuwa kumeripotiwa kiwango kidogo cha hukumu hiyo katika mataifa mengi ya Afrika.

Taifa la Guinea linakuwa la 20 chini ya mataifa yaliyo chini ya jangwa la sahara kufututilia mbali hukumu ya kifo kwa makosa yote, huku Kenya ikifuta hukumu hiyo kwa kosa la mauaji.

Burkina Faso na Chad zimechukua hatua ya kurekebisha adhabu hiyo kwenye mapendekezo ya sheria mpya.

Katibu mkuu wa shirika la Amnesty, Salil Shetty, anasema kuwa, hatua zinazopigwa katika mataifa yaliyo chini ya jangwa la Sahara za kufuta hukumu ya kifo, zinaimarisha nafasi yake kama mhimili wa matumaini. Anaongeza kuwa, uongozi wa mataifa hayo unatoa matumaini kuwa adhabu hiyo ambayo ni kinyume cha ubinadamu na wa kudhalilisha unaweza kurekebishwa.

Mfano wa eneo ambalo hukumu ya kifo hutekelezwa
Mfano wa eneo ambalo hukumu ya kifo hutekelezwaPicha: Fotolia/Orlando Florin Rosu

Tumaini la mataifa mengine kufuata mkondo

Huku serikali barani Afrika zikiendelea kuchukua hatua za kupunguza na kufutilia mbali hukumu ya kifo mwaka huu, mataifa ambayo yangali yanatekeleza hukumu hiyo huenda yakaufuata mkondo huo.

Sasa mataifa 20 barani Afrika chini ya jangwa la sahara yamefutilia mbali hukumu ya kifo kwa makosa yote, ni wakati mwafaka kwa ulimwengu kufuta hukumu ya kifo.

Shirika la Amnesty liliripoti kupungua kwa hukumu ya kifo kwa mataifa yaliyo chini ya jangwa la sahara kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2017. Ni mataifa ya Sudan Kusini na Somalia ambayo yanajulikana kwa kukutekeleza hukumu hiyo.

Hata hivyo ripoti kuwa Botswana na Sudan zimerejelea hukumu hiyo mwaka huu, shirika la Amnesty linasema kuwa hatua za mataifa hayo hayastahili kutia doa hatua pana zilizopigwa na mataifa mengine.

Huku hayo yakijiri, Gambia imesaini mkataba wa kimataifa na kushinikiza kuwa haitatekeleza hukumu ya kifo na inaelekea kufutilia mbali huku hiyo. Rais wa Gambia alianzisha mpango wa marufuku ya muda mfupi wa hukumu hiyo Februari mwaka huu.

Shirika la Amnesty limesema kuwa mataifa yaliyo chini ya jangwa la sahara barani Afrika yalirekodi matokeo chanya ulimwenguni mwaka uliopita.

 Idadi ya mataifa ambayo yamefuta hukumu hiyo sasa ni 142
Idadi ya mataifa ambayo yamefuta hukumu hiyo sasa ni 142 ulimwenguni

Shirika la Amnesty lilirekodi yumkini visa 993 vya hukumu ya kifo katika mataifa 23 mwaka 2017, ikiwakilisha kupungua kwa asilimia nne  kutoka mwaka 2016.

Hukumu chache za kifo zilitolewa 2017

Yumkini visa 2591 vya hukumu ya kifo viliripotiwa katika mataifa 53 mwaka 2017 kiwango cha chini kikilinganishwa na visa 3117 vilivyoripotiwa mwaka 2016.

Mbali na Guinea, Mongolia ilifutilia mbali hukumu ya kifo kwa makosa yote na kulifanya kuwa la 106 mwaka 2017. Ni mataifa 23 ambayo yanaendela kutekeleza hukumu hiyo, licha ya baadhi ya mataifa kadhaa kurejelea hukumu hiyo.

Baada ya Guatemala kufutilia mbali hukumu ya kifo kwa makosa yote, idadi ya mataifa ambayo yamefuta hukumu hiyo sasa ni 142. Ni mataifa 23 tu ambayo yanaendela kutekeleza hukumu hiyo idadi sawa na mwaka 2016.

Hatua muhimu pia zilichukuliwa kupunguza hukumu ya kifo katika mataifa ambayo yanatekeleza hukumu hiyo. Katika taifa la Iran, idadi ya visa vya hukumu hiyo vilipungua kwa asilimia 11 na hukumu kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya kupungua kwa asilimia 40.

 Kwa sasa yumkini watu 21,919 wanaojulikana ulimwenguni wanakabiliwa na hukumu ya kifo.

Shirika la Amnesty linasema kuwa hukumu ya kifo ni ishara ya utamaduni wa ghasia wala sio suluhisho.

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Amnesty International Press Release

Mhariri: Mohammed Khelef