1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya Mahkama ya Katiba Ujerumani

27 Februari 2007

Uhuru wa habari umetetewa na hukumu ya mahkama ya katiba iliotoka leo kwa kesi ya jarida la "Cicero" lililovamiwa na msako wa polisi.

https://p.dw.com/p/CHJI

Tabia ya kutumia waranti wa polisi kuingia kwenye dafutari za jarida kwa umbea wa kujua nani ni chanzo cha habari zilizovuja kwa jarida hilo,hakuruhusiwi na katiba ya Ujerumani.

Ndio maana leo jarida la “Cicero” limeshinda kesi yake dhidi ya kitendo cha kupekuliwa idara zake za uchapishaji .Kesi hiyo jarida hilo ilipeleka mahkamani mwaka mmoja na nusu uliopita.

Kutokana na ilani ya Idara ya kupambana na uhalifu ya Ujerumani, mshtaki wa serikali mkoa wa Brandenburg,alijaribu kugundua ni polisi gani katika idara yao waliofichua kwa muandishi wa habari wa jarida la “Cicero”-Bruno Schirra,ripoti ya siri juu ya kikundi cha kigaidi cha Al kaida.

Mshtaki wa serikali akawatuhumu wahariri wa jarida la “Cicero” kuwa eti ni wasaidizi wa watu wanaoihini serikali kwa kutoboa siri zake.

Leo lakini,katika hukumu yake juu ya mashtaka haya ,hakimu mkuu Hans-Jürgen Papier alifafanua idara za kisheria zinajitosa katika hali nyeti.

“Kufanya msako katika idara za nuandishi habari-kutokana na kuchafuliwa kwa kazi zake na athari za kutishika kwa waandishi habari waliomo humo,kunazuwia uhuru wa uandishi-habari.”

Kwahivyo,Mahkama ya katiba imekataza kitendo hicho cha washtaki wa seriali.Kusaka na kuvipekua vyumba vya arida hilo na kunyakua dafutari zake ni ruhusa tu ikiwa muandishi habari binafsi anatiliwa shaka kweli kukiuka sheria.

“si ruhusa kufanya hivyo kwa kutilia shaka- shaka tu ili kusaka habari.Ama sivyo, kinga ya uhuru wa uandishi habari hapo itakiukwa.”

Hivyo ni mkusema: si ruhusa kwa mshtaki wa serikali kumuandama muandishi habari kisheria kwa kuwa tu amechapisha waraka wa siri wa serikali.Ni ruhusa tu kumuandama muandishi habari na jarida lake ikiwa amemshawishi mshika-siri wa serikali kutoboa siri na mshtaki wa serikali akimtilia shaka zenye msingi msiri wake aliempa habari ndipo aweza kutiwa msukosuko.

Hukumu hii ya leo ilikatwa huku mahakimu 7 wakiungamkono na mmoja akiipinga.Hukumu hii inataja na kukumbusha hukumu juu ya jarida la DER SPIEGEL iliokatwa miaka 40 iliopita-ambayo inaangaliwa kama nguzo ya kusimamia uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia nchini Ujerumani.