1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi waruhusiwa kuondoka Hungary

Admin.WagnerD3 Septemba 2015

Rais wa Baraza la Umoja wa UIaya Donald Tusk ametahadharisha kwamba mgawanyiko baina ya nchi za magharibi na mashariki katika Umoja wa Ulaya unazitatiza juhudi za kuushughulikia mgogoro wa wakimbizi.

https://p.dw.com/p/1GQWL
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor OrbanPicha: picture-alliance/dpa/O. Hoslet

Waziri Mkuu wa Hungary amesema tatizo la wakimbizi ni la Ujerumani na siyo la Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels mapema leo ,Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema kuwa tatizo la wakimbizi ni la Ujerumani, kwa sababu ameeleza kwamba hakuna mkimbizi anaetaka kubakia nchini Hungary. Amesema wakimbizi hao wote wanataka kwenda Ujerumani.

Hata hivyo Waziri Mkuu Orban amesema nchi yake itazifuata sheria zote za Umoja wa Ulaya zinazohusu ulinzi wa mipaka. Bwana Orban alikuwapo mjini Brussels ili kukutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya na kuujadili mgogoro wa wakimbizi.

Waziri Mkuu huyo amekutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya wakati ambapo wakimbizi wanaendelea kumiminika kwenye kituo cha treni cha Keleti katika mji mkuu wa Hungary, Budapest. Wakimbizi na wahamiaji wanaendelea kujazana katika treni licha ya tangazo kwamba hakuna treni zinazokwenda katika nchi za maghariibi kutoka Hungary.

Nchi za Ulaya zagawanyika juu ya wakimbi

Wakati Waziri Mkuu huyo amewataka wakimbizi wasije barani Ulaya,Rais wa Umoja wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk ametahadharidha kwamba mgawanyiko baina ya nchi za magharibi na mashariki za Umoja wa Ulaya unazitatiza juhudi za kuushughulikia mgogoro wa wakimbizi. Bwana Tusk amesema mgogoro huo unazidi kuwa mkubwa. Amesema pana mgawanyiko baina ya nchi za magharibi na mashariki za Umoja wa Ulaya.

Rais wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk
Rais wa Umoja wa Ulaya Donald TuskPicha: Getty Images/AFP/M. Bureau

Ameeleza kuwa baadhi ya nchi za Umoja huo kama Hungary zinafikiria njia za kuwazuia wakimbizi na nyingine zinataka mshikamano , lakini kwa kusisitza sera ya kugawana wakimbizi katika msingi wa idadi maalumu. Rais wa Umoja wa Ulaya ametoa mwito kwa nchi za Umoja huo wa kuonyesha mshikamano katika juhudi za kuwasaidia wakimbizi na ametaka wakimbizi 100,000 wagawanywe kwa njia ya haki miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.

Wakati huu huo treni kutoka Slovakia na Jamhuri ya Czech zimeondoka katika nchi hizo na kuelekea katika mji mkuu wa Hungary ,Budapest. Na habari zaidi zinasema treni iliyojaa wakimbizi imeondoka Hungary kuelekea katika mji wa Sopron, karibu na mpaka wa Austria.

Mwandishi Mtullya Abdu.rtre,afp

Mhariri: Gakuba Daniel