1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wahamiaji yaongezeka sana Ujerumani

Admin.WagnerD3 Agosti 2015

Idadi ya wahamiaji kutoka nchi za nje wanaoishi Ujerumani imeongezeka tangu mwaka 2014 kufikia milioni 10.9. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na ofisi ya takwimu ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/1G96x
Symbolbild syrische Asylbewerber in Deutschland
Picha: picture-alliance/dpa

Takwimu mpya zinaonesha mtu mmoja katika kila watu watano Ujerumani ana historia ya uhamiaji. Idadi ya watu ambao hawatokei nchi za kigeni imepungua kwa kiwango kidogo, huku ile ya wahamiaji kutoka nchi za Umoja wa Ulaya ikiwa imeongezeka kwa kiwango kikubwa mno.

Takriban watu milioni 16.4 wenye historia ya uhamiaji walikuwa wakiishi Ujerumani mwaka uliopita, ikiwa ni asilimia 20.3 ya wakazi jumla au mtu mmoja katika kila watu watano. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na Ofisi ya Takwimu ya Shirikisho. Idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 3 baada ya 2013 na asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka 2011. Asilimia 56 ya watu hawa wana pasi ya Ujerumani, kwa mujibu wa ofisi hiyo yenye makao yake katika mji wa Wiesbaden.

Ripoti hiyo inatoa maelezo kuhusu kila mtu aliyehaia Ujerumaji kuanzia mwaka 1950 na vizazi vyao, pamoja na raia wa kigeni wanaosihi Ujerumani kama watu wenye historia ya uhamiaji. Uraia wa watu au utaifa wao hauna jukumu katika kueleza kama wana historia ya uhamiaji.

Ongezeko la matokeo kwa sehemu kubwa ni kutokana na kuongezeka kwa raia wa kigeni wanaokuja humu nchini, huku wahamiaji milioni 10.9 wakiishi Ujerumani mwaka 2014, idadi inayoelezwa kuwa kubwa kabisa tangu uhesabuji ulipoanza mwaka 2005.

CSU Parteitag 2014 - Angela Merkel und Horst Seehofer
Horst Seehofer na kansela Angela MerkelPicha: Getty Images/C. Stache

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji kutoka nchi zilizo katika Umoja wa Ulaya. Wakati huo huo, takwimu zilizochapishwa leo zimeonesha kwamba idadi ya watu wanaoishi Ujerumani ambao hawana historia ya uhamiaji imepungua kwa 885,800 au asilimia 1.4 tangu mwaka 2011.

Ripoti ya leo imeonesha tofauti mbalimbali zilizopo katika kiwango cha elimu cha wahamiaji Ujerumani. Mwaka 2014 asilimia 18 ya wahamiaji waliosihi Ujerumani hadi mwaka 1990 walifaulu kumaliza masomo ya elimu ya juu, lakini asilimia 43,7 kati ya wale walioanza kuishi humu nchini tangu mwaka 2011. Hata hivyo asilimia 27,8 ya wale walioanza kuishi mwaka 2011 hawakusomea taaluma, idadi ambayo ni kubwa kuliko ile ya wale wenye historia ya uhamiaji.

Mjadala kuhusu sheria mpya ya uhamiaji

Kwa sasa kumekuwa na mjadala kuhusu umuhimu wa sheria mpya ya uhamiaji Ujerumani kwa lengo la kulikabili wimbi la wahamiaji. Chama cha Social Democtaric,SPD, kinaunga mkono sheria ya aina hiyo, lakini washirika wake serikalini, muungano wa chama cha Christian Democratic Union, CDU, cha kansela Angela Merkel, na chama ndugu cha Christian Social Union, CSU, wamegawanyika. Ikiwa chama cha CDU kitakuwa wazi kulikubali wazo hilo, bila shaka chama cha CSU kitaipinga.

Jambo lililowazi ni kuwa: Haiwezekani kulisuluhisha tatizo la uhaba wa wafanyakazi Ujerumani kwa kutumia haki kwa wahamiaji - hayo ni mambo mawili tofauti kabisa, na hili wanalifahamu fika viongozi wa chama cha CSU," amesema Peter Altmeier, wa chama cha CDU, waziri katika ofisi ya kansela, katika gazeti la leo la Bild.

Katika maohojiano yake ya wakati wa msimu wa kiangazi na kituo cha televisheni cha ARD, Horst Seehofer, mwenyekiti wa chama cha CSU, alisema mwishoni mwa juma, "Sheria ya uhamiaji itakayoruhusu wahamiaji zaidi kuja Ujerumani halitakuwa suala la kujadiliwa na chama."

Mwandishi: Josephat Charo/dw.com/english

Mhariri: Mohammed Khelef