1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wasiokua na ajira yapungua Ujerumani

A Mtullya4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ck7q

NUREMBERG.

Idadi ya watu wasiokuwa na ajira imeendelea kupungua nchini Ujerumani kutokana na ustawi thabiti wa uchumi.Idara kuu ya ajira ya mjini Nuremberg imasema idadi yawatu hao ilipungua kwa alfu 78 mwezi uliopita.

Idadi hiyo inawakilisha asilimia nane nukta moja ya watu milioni 3 na laki tano ambao kwa sasa hawana ajira hapa nchini.

Serikali ya Ujerumani imeeleza kuwa takwimu hizo zinathibitisha mafanikio ya sera zake za mageuzi. Waziri wa ajira bwana Scholz amesema jerumani imeingia katika mwaka mpya ikiwa na matumaini makubwa.