1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IGAD yaahirisha mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini

19 Aprili 2018

Jumuiya ya IGAD iliyotarajiwa kuwa na mazungumzo mapya April 26 pamoja na vyombo vingine vya kimataifa kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani imekuwa ikitafuta njia ya kupatikana suluhu kati ya pande mbili zinazozozana

https://p.dw.com/p/2wJPa
Südsudan Präsident Salva Kiir
Picha: Reuters/T. Negeri

Jumuiya ya ushirikiano wa nchi za pembe ya Afrika IGAD imesema kuwa imeahirisha mazungumzo ya mwezi huu yanayolenga utekelezaji wa mkataba wa amani wa Sudan Kusini ikiwa ni hatua ya hivi karibuni ya kukomesha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu nchini humo kwa miaka minne.

Licha ya makubaliano kadhaa pamoja na usitishwaji mapigano bado mgogoro nchini Sudan Kusini umekuwa ukiendelea tangu mapigano yalipoibuka mwishoni mwa 2013 ikiwa ni miaka miwili baada ya nchi hiyo kupata uhuru.  Jumuiya ya IGAD iliyokuwa inatarajiwa April 26 kuwa na mazungumzo mapya pamoja na vyombo vingine vya kimataifa kuhusiana na utekelezaji wa mkataba huo imekuwa ikitafuta njia ya kupatikana suluhu kati ya pande mbili zinazozozana nchini humo ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi wa waasi Riek Machar.