1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ILULISSAT: Merkel akamalisha ziara ya Greenland

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYC

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ameikamilisha ziara yake ya siku mbili kisiwani Greenland kwa kutoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuhifadhi mazingira.Amesisitiza umuhimu wa juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka hii ijayo.

Wakati wa ziara yake kisiwani Greenland,Kansela Merkel amejionea vipi barafu inavyozidi kuyayuka kwa haraka kwa sababu ya ongezeko la joto duniani.Hata wakati wa ziara ijayo ya Merkel nchini China na Japan,suala la kuhifadhi mazingira litapewa kipaumbele.